Pages

Wednesday, December 25, 2013

USHAURI KWA VIJANA WA KITANZANIA

Hakuna mtu asiyependa utajiri lakini utajiri unaweza kupatikana bila kufanya biashara haramu au kujihusisha na mambo ya kuhatarisha maisha yako. Kwa miaka ya karibuni kumekuwa na Watanzania wengi wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya na wanaofaidika ni wachache tu wengi wao wanaishia kupata pesa ndogo na wanahatarisha maisha yao kwa kufugwa, kifungo cha kifo na hata madawa kupasuka tumboni na kuwaua. Kabla hujapata utajiri wa kudumu unatakiwa kupenda maendeleo kwanza na sio sifa pekee kwenye jamii. Fanya yafuatayo na polepole utafanikiwa.

1. Tafuta mtu ambaye unataka kuwa kama yeye: Usiangalie ukabila udini wala rangi ya mtu. Kama unataka kuwa kama Mengi, Mkono, Manji, Wanasiasa, wasomi au hata wasomi wa kimataifa wanaofanya kazi kwenye UN, World bank, diasporas. Tafuta mtu mmoja au wawili na waombe wawe kama walimu wako. Usiogope kutafuta utapata mtu na fuata wanayo kuambia hata kama wewe huoni umuhimu kwa sasa.

2. Jiendeleze kielimu: Hakuna mtu ambaye hawezi kufanya hili hata kama ni polepole. Elimu sio lazima iwe ya degree kwani duniani sasa kazi zinazolipa hazifundishwi kwenye degree bali certification mfano sasa tuna gas jifunze ufundi wa machine za kuchimba mafuta, project management, computer language, database kama SAP,Oracle, dot.net. Vilevile kuna Veta tafuta kitu ambacho kinauhusiano na Gas na Oil. Kwa ujumla jiwekee utamaduni wa kujiendeleza.

3. Marafiki: Tafuta marafiki ambao wanakusaidia kujiendeleza na wanakupenda badala ya wale wanaotaka kukutumia na wanao ku support kinafiki. Kama huna marafiki wazuri tafuta uhusiano wa kuomba kama mtanzania mwenzako omba urafiki kama Watanzania walivyokuwa wanafanya miaka ya zamani. Marafiki wabaya watakupeleka jela na kukuingiza kwenye ushabiki wa kimaisha na kukutumia.

4. Acha kulalamika: Kama unataka kuendelea uache utamaduni wa kulalamika badala yake jiulize je ni kitu gani naweza kufanya kufanikiwa bila kuiba. Tabia nzuri inaweza kukupeleka mbali kuliko unavyofikiri pesa pekee sio sababu ya kushidwa kuanza bali mara nyingi ni tabia. Ukiwa na tabia nzuri na kujihusisha na watu wazuri pesa haitakuwa kigezo.

5. Nenda ugaibuni kama umeshidwa yote: Kama yote umeshidwa na mazingira uliyo nayo si mazuri labda kabla ya kujihusisha na biashara haramu jitoe kwenye mazingira uliyopo. Kama bado ni kijana na mambo hayaendi yote hapo juu tafuta njia za kwenda nje lakini hayo mambo hapo juu inabidi uyafuate hata kama uko ugaibuni.

6. Uvumilivu: Hii nitakupa mfano wa ukweli kabisa. Watanzania wengi tulikuwa USA miaka ya 1996-2000 kutafuta maisha kwenda shule n.k. Watanzania wote tuliishi pamoja na mimi nilikuwa mojawapo pale Houston, TX tulifanya kazi pamoja umri ulikwa kama sawa tu kwa ufupi tulianza wote kwenye zero. Baaada ya miaka michache Watanzania wengine walihusisha na biashara, wengine shule, wengine mission town deals. Waliopiga deal walichukua pesa na kukimbia Tanzania na hawa walienda na magari, pesa na walipata wanawake, wanaume wanaowataka nyumbani. Wengi wao walienda bila kumaliza shule au kujifunza biashara. 

No comments: