KANDA NA CHADEMA NI MSINGI
Baada ya kuundwa kwa kanda ambayo ni mmoja ya mafanikio ya mwaka, ilianzishwa program ya Chadema ni msingi. Kwa ufupi hii ni program ya ujenzi wa chama ngazi ya kitongoji ambapo msingi mmoja unakuwa na viongozi na wanachama wasiopungua 30.
Ktk kikao cha Kanda ya ziwa magharibi hivi karibuni, taarifa iliyotolewa ni kuwa asilimia 48 ya vitongoji vya kana hiyo tayari ina misingi ya chama. Haya ni mafaniko makubwa sana kufanyika kwa mwaka mmoja. Na kwa kuwa program hii inaendealea mpaka Feb 20 . 2014 inawezekana kufikia 60%.
Kinachotia moyo zaidi ni kuwa program hii imefanyika huku wapinzani wetu Ccm wakiwa busy kutuchonganisha makao makuu. Nadhani hawakupima madhara ya kanda au labda mfumo wao wa ku-ditect hatari ni dhaifu. Tunasubiri taarifa rasmi ya kanda nyingine kupima mafanikio haya.
MABARAZA YA KATIBA MPYA:-
Kwa kutumia kanda chama kilisambaza fomu maalum majimbo yote nchini ili wanachama wetu watoe maoni yao kwa mchakato mpya. Kwenye jimbo naloishi mimi kwa mfano wanachama 11180 walijaza fomu hizo. Haya ni mafanikio ya kujivunia maana chama kiliwashirikisha katika suala kubwa la kitaifa.
Baada ya kujazwa kwa fomu hizo, chama kikaja na mbinu nyingine ya kukusanya maoni. Kikanyanyua Chopper mbili, moja na Dr Slaa na Marando na nyingine chini ya Kamanda Mbowe, Lissu na Mnyika. Ikapigwa mikutano nchi nzima watu wakajaa kwa maelfu (Chama kikatangazwa..
?)
Huko bungeni nako moto ukazidi kuwaka, mara mbili wabunge wakatoka nje ya bunge kushinikiza mambo wanayotaka katika sheria ya mabadiliko ya katiba. Mara mbili wakatinga Ikulu na rais akakubaliana na mapendekezo yao. Watanzania wakatambua ni chama gani kinataka katiba bora.
HATUA ZA KINIDHAMU NDANI YA CHAMA:-
Aliyekuwa makamu mwenyekiti Bavicha Juliana Shonza na wenzake walifukuzwa uanachama, huku naibu katibu mkuu Zitto Kabwe na wenzake wakivuliwa nyadhifa zao. Wengi wanalichambua suala hili ktk sura ya mgogoro lakini lina faida zake.
Kwanza limeonyesha ni chama makini kisichomwopa mtu bila kujali nafasi na umaarufu wake. Lakini kosa la Ccm kuwapokea Shonza na wenzake kulithibisha madai kuwa vurugu zinzoendelea kwenye chama chetu zinafadhiliwa na Ccm.
SUALA LA RWAKATARE NA UGAIDI:-
Itakumbukwa kuwa mwaka huu ndo tumeshuhudia mkurugenzi wetu wa usalama akibambikizwa kesi mbaya ya ugaidi. Pamoja na kiongozi mkubwa ndani ya chama kushauri Rwaks atoswe na chama sijui kwa faida gani, chama kiliamua kufa naye (shukrani kwa wanasheria wetu mahiri) Rwaks akashinda kesi na hira za wabaya zikashindwa.
Wabaya wetu hawakukata tamaa, sasa wakaona liwalo na liwe! Wakaona wammalize mwenyekiti na Lema. Wakarusha bomu kwenye mkutano pale Soweto (Chama kina ushaidi na Mkuu wa kaya). Lakini Mungu ni mwema mwenyekiti wetu na Kamanda Lema wote wakaokoka ingawa makanda wengine watoto kwa wakubwa walipoteza maisha.
Damu yao itaandika historia ya ukombozi wa mara ya pili ambayo tunapambana na ndugu zetu ambao ni wabaya kuliko wageni waliotutawala wakati huo wa ukolo ni. Lakini upande wa pili wa uzuri wa shambulizi hili, limetufundisha kwamba vita hii si lelemama bali ni mapambano kamili ya kuikomboa nchi yetu na kupigania chama chetu.
Yote haya kwangu ni mafanikio makubwa, misusuko yote tuliyopata tumeweza kupita ktk mwaka huu kwa mafanikio makubwa. Katika mwaka unaofuata mapambano yatakuwa makali zaidi maana ni mwaka wa uchaguzi serikali za mitaa, uchaguzi ndani ya chama na kupitisha katiba mpya.
Tunahitaji uongozi imara usiyoyumba utakaotuvusha katika haya na kuikomboa nchi yetu mwaka 2015. Niliwahi kuandika huko nyuma humu, kwama hatuwezi kubadali kocha timu inafanya vizuri. Tufanye marekebisho madogo kwenye safu alafu tusonge mbele.
Nawasilisha!
CHADEMA CHAMA CHETU, TANZANIA NCHI YETU.
No comments:
Post a Comment